ALIYEKUWA Mshambuliaji wa AZAM FC Prince Dube ameilipa klabu yake ya zamani Shilingi Milion 500 na sasa yuko huru kujiunga na Yanga ambayo imekuwa ikihusishwa nae tangu asuse na kuondoka Chamazi.
Taarifa za awali ziliripoti kwamba Dube ameukana mkataba aliokuwa nao na Azam FC unaoisha 2026 na akaondoka Chamazi. Staa huyo alikwenda kushtaki katika Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF) na kesi ikaanza kusikilizwa Aprili 18.
Baada ya kesi kusikilizwa na maamuzi kutoka, ilionekana mchezaji huyo amekiuka makubaliano yake kimkataba hivyo anatakiwa kulipa fidia.
Habari za Uhakika kabisa zinasema kwamba, tayari kila kitu kimefanyika kwa mchezaji huyo kuwalipa waajiri wake, na mambo yote yanamfanya awe huru kujiunga na timu yeyote.
Yanga ni moja ya klabu inayomfuatilia kwa karibu sana mshambuliaji huyo, ambaye amewavutia Wananchi na wanaitaka sana saini yake.
Inaelezwa kwamba Prince Dube alifichw mitaa ya Avic Town na Uongozi wa labu hiyo, wakati sakati zima likiendelea mpaka sasa mambo yanaelekea kuwa mazuri.
Kama mambo na dili la Prince Dube litakamilika Yanga, basi safu yao ya ushambuliaji itakuwa ya moto sana msimu ujao.
Wakti yote yanaendelea inshu ya Chama kujiunga na Yanga pia inazidi kusika kasi, ikielezwa kwamba ameshindwa kukubaliana na Uongozi wa Simba. Suala zima likiwa ni mshahara mkubwa anaoutaka kiai cha zaidi ya Mil 50 TZS.