Wakenya hawajatuzidi, ila wametuwahi: Idris Sultan

 


Mchekeshaji na mwanamitandao maarufu wa Tanzania Idris Sultan,  ametolea ufafafanuzi dhana iliyopo kuhusu tasnia ya Sanaa nchini Tanzania kuzidiwa kimaendeleo na tasnia ya Sanaa chini Kenya kwakua Kenya wanazo kazi nyingi za kimataifa kuliko Tanzania,  ambapo jibu lake likawa ni ‘Kind off’.


Idris ametolea maekezo dhana hiyo kwa kuweka wazi kuwa kwa kiwango flani Kenya wamesoge lakini bado hawajaiacha tasnia ya Sanaa ya Tanzania, ameyasema hayo alipoulizwa na chombo The chanzo, kwanini Kenya ina filamu nyingi kwenye Mtandao wa Netflix na channel ya ‘Showmax’ kwa upande wa Afrika Mashariki kwani wao wanatuzidi nini?


“Hawajatuzidi leo Kwa bahati mbaya, wametuzidi zamani kidogo na hiyo zamani ndio ime-determine leo yao na ilikua ni lugha (kiingereza) na sio kwenye kutuzidi labda kwenye kuongea, bali wamekitumia kwenye kazi zao za kisanaa, na Kenya hawaongei kiingereza tu au kiswahili tu, bali wanachanganya kiswahili na Kiingereza, hii inawasaida kua na mfanano na Mataifa mengine. Sasa unapoingia kwenye majukwaa ya kimataifa kama Netflix na Showmax ukija kutengeza maudhui, unataka uweke maudhui ambayo watu wengi katika mataifa tofauti wanaweza kuyaelewa na hapo ndipo lugha inaposaidia’ amesema Idris


Ambapo pia ametilia mkazo kuwa licha ya Wakenya kuwahi kufanya mambo makubwa kwenye sanaa mbele ya Tanzania, kwa sasa hali ni tofauti kwa sababu ukubwa wa vipaji, wasanii, uwekezaji  pamoja na vipaji Tanzania iko mbele ya Kenya.


“Kwa hiyo wao Kenya, tuseme tu walituwahi, lakin kwasasa hivi ukisema utuweke kwenye mzani mmoja na unangalie ni wapi wametuzidi kwenye Sanaa Kwa ujumla, kuanza ujuzi, vipaji na ubunifu ni wazi sisi tuko juu yao pakubwa sana kwenye sanaa Kwa ujumla wake na sio muziki wala filamu tu peke yake,” ameongeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad