Watu Waliohusika na Mauji ya Mtoto Asimwe Wakamatwa



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi limewakamata watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novath (2).

Mei 30, 2024 Asimwe anadaiwa alichukuliwa na wattu wasiojulikana nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera na juhudi za kumtafuta hazikuxzaa matunda hadi hapo Juni 17, 2024 mwili wake ulipopatikana ukiwa katika mfuko wa sandarusi huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa.

Waziri Masauni amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vithibiti vya kutendea kosa hilo na kufafanua kuwa hawajabahatisha katika kuwakamaa watu hao.

“Hakuna hata mmoja ambaye amehusika na mauaji ya binti huyu malaika wa Mungu atakayrepona, tumefikia pazuri na kitakachofanyika itakuwa fundisho kwa wahalifu wengine,, tupo vizuri katika kukabiliana na uhalifu na ndiyo maana hakuna mtu atakayefanya uhfifu asipatikane,” amesema Masauni

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad