Wema Sepetu Afunguka 'Sikuwahi Kula Hela ya Big Brother ya Idriss Sultan, Mwamba Alichanganya Ikapotea"

Wema Sepetu Afunguka 'Sikuwahi Kula Hela ya Big Brother ya Idriss Sultan, Mwamba Alichanganya Ikapotea"
 

Malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu amesema kuwa hajawahi kula hata shilingi moja ya aliyewahi kuwa mpenzi wake na mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots mwaka 2014, Idris Sultan.


Idris alishinda taji hilo na kupewa zawadi ya dola $300,000 ambazo ni takribani Tsh milioni 500 kwa kipindi hicho.


“Labda watu hawajui, ngoja niseme ukweli na watu wanisikilize kwa umakini na wanielewe. Hela ya yule kijana sijawahi kula mimi hata shilingi moja, au niingie deep niseme hela ambayo nimewahi kula ni kitu gani? Alininulia tu pafyume na Tom Ford na Vaileth Okid ndo hicho ambacho nimewahi kufaidika.


“Lakini watu wananizushia Wema alichukua hela ya yule kijana… aseme yeye kama mimi niliwahi kuchukua hela kiasi flani nikaipeleka wapi. Hicho kitu kinanikera hata yeye anashangaa kwa nini watu wananizushia, hawezi kunitetea public lakini ni vyema sasa atoke hadharani anitetee.


“Sikwenda kwa Idris kwa sababu alikuwa amepata pesa, yalikuwa mapenzi yang utu kwake, wala sikutaka chochote kutoka kwake. Yeye anajua pesa zake alipotezaje lakini sio sababu ya Wema Sepetu. Aliye-enjoy hiyo pesa ni Samantha enzi hizo, sio mimi,” amesema Wema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad