Klabu ya Yanga imesema itaanza kuanika wachezaji wapya na wale itakaoachana nao kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Aidha klabu hiyo imesema haidaiwi na mchezaji yeyote baada ya kuwalipa wachezaji waliokuwa wanadai siku moja kabla ya dirisha la usajili kwa ajili ya msimu wa mwaka 2024/2025 kufunguliwa Juni 15.
Akifanya mahojiano na kituo cha Luninga cha Azam Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema imefanya malipo ya wachezaji Lazarous Kambole na Mamadou Doumbia Juni 14.
“Baada ya kufanya malipo tukatuma uthibitisho Fifa na kilichobaki ni Shirikisho hilo kufanya malipo tukatuma uthibitisho kwa Fifa na kilichobaki ni Shirikisho hilo kufanya mawasiliano na wachezaji hao, hivyo hakuna mchezaji anayetudai” alisema Ali Kamwe.
Alisema kwa sasa Yanga hawana kesi yoyote Fifa inayohusu malipo ya wachezaji na kuhusu suala la Augustin Okrah watasubiri ripoti ya Kocha.
Katika hatua nyingine Kamwe alisema kuanzia Julai Mosi mwaka huu klabu hiyo itaweka hadharani wachezaji walioongeza mkataba wapya na wale watakaowapa mkono wa kwaheri.
“Tutaanza kusema wachezaji waliongezewa mkataba, walioachwa na wachezaji wapya” alisema Ali Kamwe