WAWAKILISHI wa Tanzania kwa upande wa mashindano ya Kimataifa, Yanga SC na Azam FC kwenye Klabu Bingwa Afrika, na Simba SC na Coastal Union watawakilisha Taifa upande wa Kombe la Shirikisho.
Yanga ni bingwa wa Ligi Kuu na Azam FC alimaliza kwenye nafasi ya pili hali inayompatia tiketi hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya miaka mingi kupita.
Yanga ni moja ya klabu inayopewa nafasi kubwa zaidi ya kufika mbali kwenye mashindano hayo, kutokana uzoefu wao wa misimu miwili ambao Azam FC hawana huo uzoefu, hivyo wanahitaji umakini mkubwa sana kuzicheza mechi hizo.
Kanuni za mashindano ya CAF, haswa kwa upande wa Ligi ya mabingwa Afrika inaeleza kwamba, endapo klabu itafungwa kwenye michezo ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa, na kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya CAF, itaondoshwa moja kwa moja kwenye mashindano hayo.
Hivyo haitoruhusiwa kushiriki kwenye mashindano ya Kombe la shirikisho kama ilivyokuwa hapo awali.
Pia kanuni za mashindano hayo inaendelea kwa kufafanua kwamba, timu zitakazofuzu kutoka hatua ya pili ya awali ya kombe la shirikisho, zitaingia moja kwa moja hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Kwa upande wa Simba SC kanuni hizo na kwa uzoefu wao jinsi ya kucheza mashindano hayo, sio shida sana kwenye kanuni hizi, wana uzoefu mkubwa sana kulinganisha na Yanga SC, Azam FC, Coastal Union.
Simba imeendelea kujiimarisha kwa kufanya sajili za wachezaji wengi, ikiwemo Elie Mpanzu, dili la Yusuph Kagoma lipo sehemu nzuri zaidi kutika, Lameck Lawi na kuna tetesi za wachezaji wengine wengi.