Yanga yaja na staili mpya ya usajili

 

Yanga yaja na staili mpya ya usajili

Klabu ya Yanga SC imekuja na staili mpya ya usajili chini ya Rais wake Injinia Hersi Said waliyoanza kuitumia ndani ya misimu hii miwili mfululizo chini ya uongozi wake imewapa makombe manne.


Timu hiyo chini ya Hersi, imeboresha kikosi chao kwa kufanya usajili wa kisasa uliowapa mafanikio ukiwemo baadhi ya Pacome Zouzoua, Yao Koaussi, Maxi Nzengeli.


Wengine ni Stephane Aziz Ki, Djigui Diarra, Kennedy Musonda na Khalid Aucho ambapo timu hiyo imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu na Mshindi wa pili katika Kombe la Shirikisho pia kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa tangu Hersi na Kamati ya Utendaji hiyo imeingia madarakani, wameingia mbinu mpya ya usajili wa wachezaji ambayo wanaifanya wakati ligi za nchi zote zinaendelea.


Kamwe alisema kuwa mbinu imewawezesha kufanya uchaguzi mzuri wa wachezaji wakati huo timu nyingine zikiwa bize na ligi wao wanakamilisha dili za usajili.


Aliongeza kuwa katika kuthibiisha hilo, wao kabla ya ligi haijamalizika usajili wao ulikamilika kwa asilimia kubwa, kilichobaki kuwatambulisha kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad