Yanga Yawaficha Mastaa Wake Ulaya, Kuanza Kutambulishwa Muda Wowote

 

Yanga Yawaficha Mastaa Wake Ulaya, Kuanza Kutambulishwa Muda Wowote

YANGA inapiga hesabu kuwaficha mastaa wake Urusi kujiandaa na msimu mpya wa kimashindano, lakini iwapo itakwama kabisa basi itatua Sauzi na ikakutana uso kwa uso na kocha wa zamani wa timu hiyo, Nasredine Nabi.

Hesabu za kwanza kwa Yanga ni kwenda Urusi kujichimbia kwa maandalizi ikiwa na mualiko wa klabu rafiki ya CSKA Moscow lakini pia mezani kwa mabosi wa klabu hiyo kuna ofa ya maana nyingine.

Mabosi wa CSKA Moscow wamefika nchini tangu jana, na kuzungumza na Uongozi wa timu hiyo, huku wakukubaliana kuwatoa baadhi ya wachezaji kwenda kucheza na kukuza vipaji vyao huko Urusi.

Inaelezwa kwamba Yanga wana oofa nyingine ya kwenda kucheza Kusini mwa Afrika, pale kwa Madiba na ndiyo kipaumbele chao cha kwanza, kwa sababu ya ukaribu na usalama pia.

Huenda kitakachowakwamisha Yanga kwenda Urusi ni sababu za kiusalama pekee ambayo nchi hiyo inapitia kwa sasa, ikiwa katika mgogoro wa kivita na taifa jirani la Ukraine, hivyo mabosi hao wanahofia kwenda huko.

Sababu nyingine inayowafanya Yanga kujichimbia Afrika ya Kusini na sio Urusi, ni hali ya hewa ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, hivyo itaendana na programu zao za mazoezi chini ya Miguel Gamondi.

Inaelezwa kwamba kila  kitu kuhusu maandalizi yamsimu  ujao kipo tayari,  na muda wowote Yanga watatangaza taarifa ya kikosi chao kuingia kambini kwaajili ya Pre Season.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad