AFISA Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally ameibuka na mpya baada ya kusambaa sana kwa habari za usajili wa Chama kwenda anga.
Ahmed Ally amesema kwamba klabu hiyo imeshakamilisha usajili wa wachezaji wengi wa kimataifa, na baadhi yao wanatoka nchi za mpira kama Zambia, DR Congo na Ivory Coast.
“Tuna wachezaji wapya saba wa kigeni wapo hapa hapa Tanzania kwa ajili ya usajili, bahati nzuri si watu wengi wanaowafahamu, lakini pia wapo chini ya ulinzi mkali, napenda kuwaambia Wanachama na Mashabiki wa Simba wasione kimya wakadhani hakuna kinachofanyika,
“Wakati haya majembe saba yapo Dar, baadhi ya viongozi wetu wamegawana majukumu, kuna mmoja yuko Zambia, yupo aliyekwernda lvory Coast, kuna anayesafiri kwenda DRC (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), mmoja Maylasia, kote huko wanakwenda kumalizana na wachezaji,
“Tumefanya ukarabati mkubwa, timu hii lazima tuijenge upya, watu wamechoka, wanataka furaha, wanataka Makombe, hawataki kuendelea kuyaona ya zamani, wanataka kuyaona mapya, huwezi kuyapata kama hujatengeneza timu Bora.” -Amesema Ahmed Ally.
Simba imefikia hatua ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wao Raia wa Zambia, Clatous Chama ambaye amesajiliwa Yanga na kutambulishwa Asubuhi ya leo Julai 1, 2024.
Inaelezwa kwamba tajiri wa klabu ya Simba Mo Dewji alifanya jitihada kubwa za kumbakiza Unyamani Clatou Chama, lakini haikusaidia kwani mchezaji huyo alitaka dau kubwa zaidi ya usajili.
Chama alivyofika kuzungumza na muwekezaji Mo Dewji aliongeza dau tofauti na kiwango cha pesa alichokitaka wali, sasa alihitaji Tsh Milioni 830 na mshabara wa Tsh Mil 40.
Hali hiyo iliwafanya mabosi wa Simba kurudi nyuma na kuachana nae, na sasa wapo sokoni kutafuta mbadala wake ambapo wanahusishwa zaidi na Kiungo wa Stella D’abjen Jean Charles Ahoua.