Ahmed Ally "Kibu Denis Akitoa Bilioni 2.7 Tunamuachia Aende Timu Yoyote"



Kibu Denga sijapewa status yake mpya, taarifa niliyokuwa nayo ya mwisho ni kwamba tunamtambua kama mtovu wa nidhamu ambaye hajaripoti kazini mpaka muda huu na klabu itachukua hatua za kinidhamu kulingana na miongozo yetu.

"Sijapata taarifa mpya kuhusiana na Kibu Denis kitu gani kinaendelea kwa upande wake lakini taarifa ya mwisho ndio hiyo tutamchukulia hatua za kinidhamu.

“Yapo maneno mengi yanayosemwa, mimi siwezi kuyasema hayo kwa sababu bado hayajawa rasmi katika dawati langu la habari lakini ni muhimu watu wakaelewa kwamba Kibu ni mchezaji halali wa Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili na bado hajaanza hata kuutumikia, bado ni mbichi vibaya mno na ana jukumu la kuutumikia.

“Kama ilivyo mikataba mingine kote duniani mkataba wake unaruhusu kuvunjwa kwa maana anao uwezo wa mchezaji wa kuuvunja mkataba wake.

“Kama anahitaji kununua mkataba wake basi anatakiwa kuweka mezani dola milioni moja, akiiweka hiyo hapigiwi hata simu, sawa na shilingi Bilioni 2.7 za kitanzania."- Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad