AJALI:Treni ya mizigo yapata ajali Morogoro

 

AJALI:Treni ya mizigo yapata ajali Morogoro

Treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania imepata ajali eneo la Bigwa, mkoani Morogoro.


Ajali hiyo imetokea saa 12 jioni ya jana Jumatatu, Julai 29, 2024 ambapo mabehewa matano kati ya 20 yaliyokuwa yamebeba ngano yamepinduka na hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokea.


Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Stesheni Masta msaidizi wa Morogoro, Godfrey Temba amesema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika.


"Mafundi wanaendelea na uchunguzi kubaini sababu halisi ya ajali hii," amesema Temba.


Temba amewahakikishia wananchi hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea kutokana na ajali hiyo.


"Tunashukuru hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa katika tukio hili," amesema.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad