Alex Msama Apandishwa Kizimbani Mashtaka ya Kugushi

 

Alex Msama
 Alex Msama

 Alex Msama Apandishwa Kizimbani Mashtaka ya Kugushi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo Julai 9, 2024 imesikiliza Kesi ya Jinai namba 275 ya mwaka 2022 inayomkabili Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama Mwita mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Isihaka Kupwa.


Msama ambaye anakabiliwa na mashitaka manne ambayo ni mashitaka kughushi nyaraka mbalimbali na sahihi za muziano pamoja na kuwasilisha nyaraka hizo za uongo kinyume na Sheria ya kanuni ya adhabu.


Katika Shitaka la kwanza la Kughushi, Alex Msama anadaiwa siku isiyojulika ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kufanya udanganyifu alighushi nyaraka za mauziano yenye Tarehe ya Julai 6, 1970, akikusudia kuonyesha kuwa ni nyaraka halisi za mauziano kati ya Khalid Swalee Chengu na Ndelikyama Mweleli huku akijua fika kuwa ni za uongo.


Katika Shitaka la pili la kughushi, inadaiwa Aprili 24, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam Kwa nia ya kufanya udanganyifu, anadaiwa kughushi sahihi ya Ndelikyama Mabolio Mweleli katika Mkataba wa mauzo wa Aprili 24, 2016 Kwa kusudi la kuonyesha kuwa ni nyaraka halisi za mauziano kati yake na Ndelikyama Mabolio Mweleli, huku akijua wazi kuwa ni uongo.


Aidha, Katika Shitaka la tatu la kughushi, inadaiwa Siku ya Aprili 24, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam, Kwa nia ya kufanya udanganyifu, alighushi barua ya ofa yenye kumbukumbu namba D/KN/A/13504/TMM yenye Tarehe ya Septemba 28, 1979 na jina la Ndelikyama M. Mweleli, Kwa kusudi la kuonyesha kuwa Kiwanja namba 160 kilichopo Mbezi Beach Dar es Salaam, kilikuwa ni Cha Ndelikyama Mabolio Mweleli huku akijua wazi kuwa ni za uongo.


Katika Shitaka la nne la kuwasilisha nyaraka za uongo, Msama Anadaiwa, kati ya Aprili na Oktoba 2016 katika Mahakama ya Ardhi Wilaya ya Kinondoni iliyopo mwananyamala Dar es Salaam, Kwa kujua na Kwa lengo la kulaghai, alitoa nyaraka za mauzo za Aprili 2016 kati yake na Ndelikyama Mabolio Mweleli katika Mahakama hiyo Kwa kusudi la kuonyesha kuwa ni nyaraka halisi za mauziano huku akijua kuwa ni za uongo.


Hakimu Mfawidhi Isihaka Kupwa akiahirisha shauri hilo hadi Jumatatu ya Julai 15, 2024 Kwa ajili ya kuendelea kusikiliza ushahidi wa Kesi hiyo Kwa upande wa Jamhuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad