Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Shaban Kamwe amesema kuwa klabu ya Yanga haina kamati ya usajili kama ambavyo watu wengi wanadhani bali usajili wao umefanyika kwa mapendekezo na ripoti ya Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi.
“Kwanza Yanga haina kamati ya usajili tumeshavuka kuwa na kamati hizo kwenye timu yetu, Yanga sasa hivi inafanya kazi kitaalamu ina wataalamu kwenye kila eneo hatuna kamati ya usajili, Usajili wote ambao umefanyika umefanyika chini ya maelekezo ya Kocha wetu Miguel Gamondi”
Ally Kamwe ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Sports Arena Wasafi Media.