BREAKING NEWS:Dili la Kibu Denis na Timu ya Norways Limekufa



BREAKING NEWS:Dili la Kibu D na Kristiansund BK limekufa❌

Yes! Dili la Kibu D na timu ya ligi kuu ya Norway,Kristiansund BK,limekufa Baada ya Simba kumtaka mchezaji huyo arejee nchini Mara moja.

Mwanzoni Simba walikuwa kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Kristiansund BK,na walikuwa tayari kumuachia mchezaji huyo Ila ghafla Simba wakawatumia email Kristiansund BK ya kuwajuza Kibu hauzwi Tena…hii ni Baada ya kuhisi kuna kitu kinaendelea kutoka kwa majirani zao wa Kariakoo.

Baada ya email hiyo Kristiansund BK waliogopa kuendelea na mchakato wa Kibu badala yake wakamtaka amalizane na Simba Kisha wao watamsajili.

Hivi Sasa Kibu yuko safarini na Muda wowote atatua Dar es salaam.

Simba wamemtaka mchezaji huyo arudi Dar es salaam,ili mazungumzo na Kristiansund BK yafanyike Akiwa hapa.

Kwa bahati mbaya Kibu anarudi Bongo Ila hayuko tayari kuichezea Tena Simba,akili na mwili wake tayari viko sehemu Nyingine.

Kwa mwendelezo wa habari hii follow @usajili_na_hansrafael14 ili kujua zaidi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad