BREAKING: Rais Kagame wa Rwanda Ashinda Uraisi Tena Kwa Kishindo


BREAKING: Rais Kagame wa Rwanda Ashinda Uraisi Tena Kwa Kishindo

Rais was sasa wa Rwanda ambaye amegombea tena Urais akitetea kiti chake kupitia Chama cha RFP, Paul Kagame ameshinda tena kiti hicho baada ya kupata kura 7,099,810 sawa na asilimia 99.15 ya kura zote zilizopigwa huku akiwaacha mbali Wagombea wenzake wawili Frank Habineza na Philippe Mpayimana.

Frank amepata kura 38,301 sawa na asilimia 0.53 na Mpayimana amepata kura 22,753 sawa na asilimia 0.32.

Rais Kagame sasa ataongoza Rwanda kwa muhula wa nne akiwa ameliongoza Taifa hilo la Afrika Mashariki tangu mwaka 2000 ambapo mwaka 2015 zilifanyika kura za maoni ambazo ziliondoa ukomo wa mihula miwili ya kikatiba kwa Marais wa Nchi hiyo na uchaguzi uliofuata wa mwaka 2017 Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98.8%.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad