#BREAKING: Simba wamtambulisha Awesu Awesu

#BREAKING: Simba wamtambulisha Awesu Awesu


Klabu ya Simba imetambulisha kiungo mshambuliaji Awesu Awesu kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.


Awesu amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru baada ya kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu.


Mbali na KMC, Awesu amewahi kutimikia timu za Kagera Sugar, Azam FC na Mwadui FC kwa nyakati tofauti.


“Tumefanya marekebisho makubwa ya kikosi kwa kusajili nyota wapya ndio maana tunaongeza na wachezaji wazawa wenye ubora,”


“Kuelekea msimu mpya wa mashindano tunaandaa kikosi imara ambacho katika kila nafasi kutakuwa na wachezaji wenye ubora unaolingana.” Imeandika taarifa ya Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad