Dawa ya Kuzuia Kuzeeka Yapatikana, Wanasayansi Wafanyia Majaribio

 


Dawa ya kuzuia kuzeeka ambayo inaweza kusaidia Watu kuishi maisha marefu na yenye afya inakaribia kuja hivi karibuni baada ya Wanasayansi kuongeza muda wa kuishi kwa Mamalia (panya waliofanyiwa uchunguzi) kwa asilimia 25.


Chuo cha ‘Imperial’ nchini Uingereza, kimegundua kuwa kuzima protini inayoitwa ‘interleukin 11’ (IL-11) kunazuia saratani, kuboresha uwezo wa kuona na kusikia, na kuboresha metaboliki, afya ya mapafu na utendaji kazi wa misuli katika panya wa umri wa makamo.


Inaweza hata kuzuia upotezaji wa nywele na kuwa na mvi, video zilizotolewa na ‘Imperial’ zimeonesha panya ambao hawajatibiwa wakiwa na mabaka na mvi kwenye manyoya yao, kupoteza nywele na kuongezeka uzito huku panya waliotibiwa wakionekana vizuri na wanaong’aa.


Panya waliotibiwa pia waliishi kwa wastani wa wiki 155, ikilinganishwa na wiki 120 katika panya ambao hawajatibiwa, Prof Stuart Cook, kutoka Maabara ya baraza la utafiti wa kimatibabu la sayansi ya tiba, huko ‘Imperial’, amesema “matokeo haya yanasisimua sana.”


“Utafiti huu ni hatua muhimu kuelekea kuelewa vizuri kuzeeka na tumeonesha kwa panya, tiba ambayo inaweza kupanua uzee wenye afya, kwa kupunguza udhaifu na udhihirisho wa kisaikolojia wa uzee.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad