Dili la Mchezaji Max na Kaizer Chiefs Kocha Gamondi Aingilia Kati

 

DILI LA MAXI NA KAIZER…GAMONDI AINGILIA KATI     Share  Habari za Yanga- Maxi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ni kama amefunga mjadala juu ya dili la Maxi Nzengeli anayetajwa kutakiwa na Kaizer Chiefs akisema hakuna mchezaji yeyote wa kikosi hicho atakayeondoka, huku akichekelea ushindani wa namba ulivyo mkali ndani ya timu hiyo iliyokuwa uwanjani jana jioni kucheza na TS Galaxy.

Hapo awali kulikuwa na habari kuhusu nyota huyo kiraka kutakiwa na Kaizer ya Afrika Kusini iliyogonga hodi kwa Yanga kutaka kumsajili licha ya kuwa bado ana mkataba na kikosi hicho.

Hata hivyo, akizungumza na Mwanaspoti jana, Gamondi alisema kwa sasa hakuna uwezekano wa kumuuza mchezaji yeyote wa kikosi hicho, kwani hesabu alizonazo kwa msimu ujao zimekwisha kumalizika.

Gamondi alisema hakuna hatua kama hiyo na hawezi kuiruhusu kwa sasa na sio kwa Maxi tu, ila yeyote ambaye wameshamsajili na tayari yupo katika kikosi hicho na ameshaanza maandalizi ya msimu ujao.

“Sitakubali kumkosa mchezaji ambaye yuko katika kikosi kwa sasa, ruhusa pekee nitakayotoa ni pale atakapokosekana kwa sababu za majeraha na sio kumuuza,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Kikosi tulichosajili ni kwa malengo yetu ya msimu ujao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na ya ndani, hivyo haiwezekani kumpunguza hata mmoja, ijapokuwa nafahamu zinakuja ofa nyingi kwa wachezaji wetu nyota, lakini hatukuruhusu waondoke na badala yake tulipambana kuwabakiza ili kulinda hesabu za msimu ujao.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad