Donald Trump Aibua Mapya Kujitoa Kwa Joe Biden Mbio za Urais



Chama cha Democratic nchini Marekani, kimeanza mbio za kuteua atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba, baada ya Rais Joe Biden kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho jana Jumapili, na kumpendekeza makamu wake Kamala Harris kupambana na Donald Trump wa Republican.

Mgombea wa Chama cha Republican, na aliyetarajiwa kupambana na Biden kwenye uchaguzi wa Novemba, Donald Trump, alikuwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo kutoa maoni yao kufuatia hatua hiyo ambaye aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba Joe Biden "hakupaswa kugombea" muhula wa pili.

Hata hivyo Trump Hakuachia hapo, bali pia alihoji uwezo wa Biden kuongoza nchi katika muda uliosalia huku Biden akisema, ingawa anajitoa lakini bado atabakia White House hadi mwishoni mwa uongozi wake Januari 20, 2025.

Mengi yameendelea kuzungumzwa kufuatia hatua hiyo ya Biden, ambaye alikabiliwa na shinikizo kubwa hivi karibuni la kujiengua kutokana na wasiwasi uliozidi kuhusiana na uwezo wake wa kuongoza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad