DROO YA CAF: Yanga Kuanza na Timu ya Burundi Klabu Bingwa Afrika

 

DROO YA CAF: Yanga Kuanza na Timu ya Burundi Klabu Bingwa Afrika

Droo ya hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika imechezeshwa leo na timu zote zimepangwa.


Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo, Klabu ya Yanga wamepangwa kucheza na Vital'O ya Burundi ambapo Yanga SC wataanzia ugenini na kumalizia nyumbani.

Yanga akitoboa kwenda hatua ya pili atakutana mshindi kati ya SC Villa ya Uganda vs Commercial Bank ya Ethiopia.


Azam FC wao wamepangwa kucheza na APR FC ya Rwanda ambapo Wauza Ukwaju hao wataanzia nyumbani na kumalizia ugenini.


Aidha, Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, JKU wao wataanzia nyumbani dhidi ya Pyramids ya Misri anayoichezea Fiston Mayele.


Iwapo Azam atatoboa kwenda hatua ya pili atakutana na mshindi kati ya JKU vs Pyramids.


Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 - 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 - 25, 2024.


Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad