Gamondi Atamba: Ninawasoma Vital'O, nataka tuwapiga nje ndani

 

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa jambo analotaka ni timu yake kutinga hatua ya makundi kwanza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kabla ya mambo mengine kuendelea, hivyo anao wajibu wa kufanya vizuri kwenye hatua za awali ili afikie makundi.


Gamondi amesema kuwa anajiandaa kutoa kipigo kizito kwa Vital'O ya Burundi ambao wamepangwa nao kwenye hatua ya kwanza ya mtoano kabla ya kwenda kukutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda dhidi ya Commercial Bank ya Ethiopia.


"Hakuna kingine zaidi ya kushinda na kwenda hatua inayofuata. Kila mechi tunataka kushinda, hii ni knockout stage tutacheza nyumbani na ugenini lazima tushinde mechi zote ili twende mbele, malengo yetu ya kwanza ni kwenda hatua ya makundi.


"Hii ndiyo sababu iliyonifanya nikaja hapa msimu uliopita na ndiyo sababu iliyonibakisha msimu huu kwa sababu ninataka kupambana kwenye mashindano makubwa Afrika na kuwaonesha kuwa Tanzania inaweza kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa Afrika hususani CAFCL.


"Sijawahi kucheza na timu yoyote ya Burundi lakini nilishawahi kufika Burundi kutazama mechi moja ya timu ya Taifa ya Burkina Faso. Kwa sasa tutaanza kuifanyia uchunguzi na kuwasoma kimbinu Vital'O na nchi ya Burundi kwa ujumla.


"Kwa vile sio mbali ninaamini Wananchi watakuwa wengi huko Burundi kama walivyofanya msimu uliopita walipotufuata Rwanda wakati tukicheza na El Merrikh," amesema Gamondi.


Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 - 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 - 25, 2024.


Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad