Haya Hapa Ndio Malalamiko ya Baadhi ya Wanachama wa Yanga Kwa Bodi ya Wadhamini


Haya Hapa Ndio Malalamiko ya Baadhi ya Wanachama wa Yanga Kwa Bodi ya Wadhamini

Ukisoma nakala ya hukumu Wanachama waliopeleka kesi Mahakamani wana malalamiko kadhaa ikiwemo lawama zao kwa Bodi ya Wadhamini kuwa wapo pale hawatetei maslahi ya klabu, moja kati ya malalamiko ni kuwa:

1- Wamesikia Viongozi wana mchakato wa kwenda kuchukua mkopo kwenye benki ya CRDB na dhamana ni jengo moja la klabu linalopatikana kwenye Mtaa wa Mafia, wao wameshangazwa sana na jambo hilo hao Wanachama.

2- Hawaridhishwi kuongozwa na Viongozi ambao hawana uhalali wa Kikatiba kusimama kama Viongozi wa Yanga kwa mujibu wa Katiba yao ya mwaka 1968 iliyorekebishwa 2011, wanasema Klabu inaongozwa kimabavu na hawasikilizi Wanachama kutokana na nguvu yao kiuchumi.

3- Kwa mchakato ulivyo Viongozi wote wa Yanga tangu mwaka 2000 mpaka sasa hawakuwa Viongozi halali kikatiba, maana yake kwa mujibu wa Walalamikaji Katiba yao ilikuwa inakanyagwa eidha kwa kujua ama kutojua.

4- Wanataka Viongozi waliyopo sasa madarakani waachie ngazi wote pamoja na kukabidhi taarifa ya mapato na matumizi ya klabu ikiwa ni takwa la Kisheria nje na hapo Rais anaweza kufunguliwa kesi.

Hayo ni sehemu ya mambo ndani ya Nakala ya Hukumu hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad