Alhamisi Aprili 18, 1963: Gazeti likimuonesha Bi. Jean Conrad, Afisa biashara wa Mansfield Telephone Co., akiwa na simu ya mfukoni isiyotumia waya ambayo alisema Mansfielders wataibeba siku moja. Simu hii bado iko katika hatua ya majaribio na bado iko siku za mbali zijazo.
Watu wengi wa mji wa Mansfield kitongoji cha Nottinghamshire, Uingereza, siku hii walichukulia kuwa ni kituko wakati gazeti hilo la Mansfield News-Journal lilipoandika makala yenye kichwa cha habari: "SIKU MOJA UTAWEZA KUBEBA SIMU YAKO MFUKONI"
Katika makala hiyo, gazeti hilo likaendelea: Siku moja wana Mansfield watakuwa wakibeba simu zao kwenye mifuko yao. Hata hivyo, usitarajie kuwa itapatikana kesho.
Frederick Huntsman, meneja wa biashara wa kampuni hiyo ya simu alinukuliwa akisema: "Simu hii iko siku za mbali sana zijazo - kibiashara. Hivi sasa, ipo katika majaribio ya maabara, ila hilo linaweza kutekelezeka, ikiruhusu mtumiaji kupiga na kujibu simu popote alipo.
Simu ya kwanza ya mkononi ilionyeshwa na Martin Cooper wa Motorola katika Jiji la New York mnamo Aprili 3, 1973 kwa kutumia simu yenye uzito wa Kilo 2!
Mnamo 1979, Nippon Telegraph na Telephone (NTT) ilizindua mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Japani. Na mnamo 1983, DynaTAC 8000x ilikuwa simu ya rununu ya kwanza iliyopatikana kibiashara.
Kuanzia 1983 hadi 2014, usajili wa simu za mkononi ulimwenguni ulikua zaidi ya bilioni saba; kutosha kutoa moja kwa kila mtu duniani. Katika robo ya kwanza ya 2016, watengenezaji wakuu wa simu maarufu duniani kote walikuwa Samsung, Apple na Huawei; mauzo ya simu hizo iliwakilisha asilimia 78 ya jumla ya mauzo ya simu za mkononi.
Kuanzia 2016, chapa zilizouzwa zaidi zilikuwa Apple Iphone, Samsung, Nokia na Alcatel.
Leo, simu hizo zinapatikana kote ulimwenguni, na karibu nusu ya nchi za ulimwengu, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanamiliki angalau moja.
Kampuni ya kwanza kutoa huduma za simu za mkononi nchini Tanzania ilikuwa TIGO (Mobitel) mwaka 1994. Takriban miaka 21 toka uzinduzi wa simu ya kwanza.
Kampuni ya Tritel, ambayo haifanyi kazi tena, ilikuwa ya pili kutoa huduma hiyo.
#makinikiayahabari