Hili Hapa Kosa Kubwa Wanalofanya Timu za Bongo Kwa Wacheza Vinara Wanapokaribia Kumaliza Mikataba



Kuna kosa kubwa ambalo linafanywa na timu zetu kwa wachezaji wake. Kusubiri hadi mkataba unamalizika kabisa ndipo wanaanza mazungumzo. Kimetokea kwa wachezaji wengi. Unakumbuka ya Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajibu? Yalikuwa ni kituko kingine. Niyonzima alimaliza mkataba na Yanga. Kumbe bado walikuwa wanahitaji. Baada ya msimu ndipo wakaanza kuhangaika naye. Kumbe alishasaini Simba, akaenda zake.
.
Ajibu naye alimaliza mkataba na Simba. Hawakuona umuhimu wa kumpa mkataba mpya kabla msimu haujamalizika. Akasepa zake kwenda Yanga. Sinema ikaishia hapo. Ni kama ilivyokuwa kwa Yanga na Fiston Mayele mwaka jana. Yanga waliacha Mayele akamaliza mkataba ndipo wakaanza kubanana naye asaini mkataba mpya. Yaani mchezaji aliyefunga mabao 16 katika mwaka wake wa kwanza unaachaje kumwongeza mkataba? Ni ajabu. Matokeo yake Mayele akaondoka bure kwenda Pyramids ya Misri, akiwa kinara wa mabao kwa misimu miwili mfululizo. Msimu wake wa mwisho alifunga mabao 17 akiwa Mfungaji Bora na huko CAF alifunika pia na mabao 14, yakiwamo saba ya Kombe la Shirikisho Afrika yaliyompa tuzo ya Afrika.

Ni kama haya ya Aziz Ki pia. Hakua amepewa mkataba mpya hadi mwishoni mwa msimu. Akawa huru. Yanga wakaanza kuhaha. Matokeo yake wametoa fedha nyingi kupita kiasi kumbakisha. Anakua mchezaji ghali zaidi kwenye Ligi yetu. Sasa turejee kwenye sakata la Chama. Simba walifahamu Chama anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu. Wala hawakuhangaika kumpa mkataba mpya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad