Inshu ya Kibu Denis Kizungu Mkuti, Simba Yadaiwa Kutaka Bilioni Mbili Kumwachia

Inshu ya Kibu Denis Kizungu Mkuti, Simba Yadaiwa Kutaka Bilioni Mbili Kumwachia


Sasa kuna habari mpya kumhusu Mchezaji huyo  ambaye ametorokea Ulaya katika nchi ya Norway, kufanya majaribio na kuanza maisha mapya.

Klabu ya Kristiansund BK ya Norway wameandika barua kwa Simba SC wakimuomba Kibu Denis kwa majaribio, wamekiri kwamba hawakuambiwa ukweli kuhusiana na mchezaji hali iliyopelekea wao kufanya makosa ya kuwasiliana na kumtumia mwaliko mchezaji mwenye mkataba unaozidi miezi 6 bila kwanza kuwasiliana na klabu na kupata ruhusa kuwaliana na mchezaji na kumtumia huo mwaliko.

Wamekiri pia kukiuka taratibu na kanuni za FIFA na wameiona hatari iliyopo mbele yao. Simba SC wao wako tayari kumuachia Kibu Denis aondoke ila wanataka kipengele cha kuuzwa mchezaji kifikiwe tu ambacho ni dola za Kimarekani milioni 1 ($1M) ambacho ni sawa na bilioni 2.7 za Kitanzania (Tshs 2.7B).

Simba hawataki kusikia kuhusu majaribio kwakuwa kuna kukosa na kupata, ikitokea akakosa na kurudi manake watakuwa wametoa mwanya kwa wachezaji wao kuondoka kihuni.

Kristiansund BK wao wanaona bilioni 2.7 ni nyingi sana wanataka suluhu na Mnyama amegoma anataka heshima yake iliyopotezwa.

Ingawa uzoefu unaonyesha Simba ni klabu ambayo inaongoza kuwaachia wachezaji kwenda nje kucheza wanapopata nafasi, hata hili pia watafikia mwisho na Kibu Denis atapata nafasi kucheza Ulaya na kutimiza ndoto zake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad