Jemedari Said "Yanga Imegeuka Kuwa Dampo la Simba, Simba Kumlilia Chama ni Ujinga"



Jemedari amesema Yanga imegeuka DAMPO la Simba sports club.

"Nimejiuliza Yanga walipanga kumtambulisha Chama kabla ya mchezaji mwingine yoyote? Uhamisho “mkubwa wa kisiasa” (Pilitical signing) unaitambulishaje, bila video, madoido na ubunifu ule ambao idara ya habari ya Yanga imezoea kuufanya na kujipatia sifa. Nini kimeharakisha hili kiasi Mwamba wa Lusaka kutambulishwa akiwa chumbani anasaini na kalamu ya ‘Biki’ akiwa na jacket la maskani na sio nguo rasmi za klabu? Habari zinasema Simba walikuwa wanajaribu kupindua meza kurudisha pesa za Yanga, wenzao wakawahi siku moja baada ya tarehe ya mkataba wake kuisha wakamtambulisha bila maandalizi almuradi wameshinda vita."

"SIMBA WAMEACHWA
Sijapenda Simba wameachwa wakati wao walikuwa na nafasi ya kumfanyia “Send off” mtu ambaye walikuwa wanamtuhumu miaka mingi, wanaumiaje kwa mtu wa namna hii? Simba wana umizwaje na mtu ambaye wamemchoka baada ya miaka 7 ya masimango na nong’ono za kuwaumiza?"

"Klabu iliyofikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na msimu uliofuata kutinga robo fainali ya Kombe la Mabingwa wa Afrika, Mabingwa wa NBC Premier League mara 3 mfululizo na Mabingwa wa CRDB BANK Confederation Cup mara 3 mfululizo, hii ni kubwa sana na imejengwa kwa muda. Kwanini imegeuzwa sehemu ya ‘kutupia’ wachezaji wanaochoka kutoka Simba SC? Tuna amini Simba hawakuwa bora kuliko Yanga kwa misimu 3 mfululizo, lakini timu bora imepokea wachezaji 3 walionekana kama mzigo Simba, Austine Okra alionekana choka mbaya Simba, Yanga wakampokea, Jonas Mkude aliachwa Simba, Yanga wakambeba, Bernard Morison wakati anatoka Yanga kwenda Simba alikuwa ‘Mali safi’ ikatokea vita, siku 3 Ofisi za TFF zilifungwa kusikiliza hukumu, Morison alishinda vita hii CAS, Morison wakati anatoka Simba kwenda Yanga alikuwa ‘chokest’ hakua na jipya bahari ilikuwa shwari, leo Chama wakati wengi wakiamini hana jipya ndiyo Yanga wanaona anafaa na wanapiga hadi vigoma barabarani kumshangilia? Kwamba kweli Ganda la Muwa la jana Chungu kaona kivuno? Hii Sijapenda, Yanga ni kubwa zaidi ya hii la kugeuzwa dampo. Simba hawapaswi kumlilia Chama ni ujinga"

©️ Jemedari Said.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad