Jinsi Manabii Wanavyowakamua Fedha Waumini Makanisani Dar es Salaam


Jinsi Manabii Wanavyowakamua Fedha Waumini Makanisani Dar es Salaam

“Kama una Sh500,000 nenda pale kaandikishe jina lako uende kumuona nabii.”

Hii ni kauli ya mhudumu wa kanisa mojawapo la maombezi, akiwatangazia waumini, ikiwa ni sehemu ya kile ambacho Mwananchi limebaini katika mfululizo wa uchunguzi wake kuhusu waumini wa makanisa hayo wanavyokamuliwa mamilioni ya shilingi na viongozi wa dini ili waombewe au kubarikiwa.

Katika sehemu ya kwanza jana, tulibainisha jinsi baadhi ya makanisa jijini Dar es Salaam yanavyowafukarisha waumini kwa kuwatoza fedha nyingi kwa ununuzi wa maji, mafuta, au vitambaa, huku wengine wakilazimika kuuza mali zao.

Leo tunaangazia jinsi ilivyo vigumu na aghali kuwafikia manabii na mitume wa makanisa hayo, zikihitajika fedha nyingi kati ya Sh500,000 hadi Sh1.5 milioni na wakati mwingine hata zaidi ya hapo, huku ikielezwa kuwepo ushuhuda wa kuandaliwa ili kuuhadaa umma.

Katika moja ya makanisa ambayo yapo wilayani Temeke, ili uonane na kiongozi wa kanisa hilo, sharti utoe ada ya Sh500,000, bila kuhesabu sadaka nyingine wanazotozwa waumini.

Mwananchi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad