Kamwe Anaogopa Kufunikwa na Haji Manara Yanga?



Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe ametoka kwenye nafasi hiyo baada ya kuitumikia timu kwa miaka miwili.

Kamwe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

“A good dancer must know when to leave a stage.

“𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a j𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖..

“Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;

“Na ni hekima hii, inanituma mbele yenu wananchi, mashabiki na wanachama wa klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka jukwaani.

“Nimesimama miaka miwili juu ya hili jukwaa, tumeimba, tumecheza, tumefurahi na Alhamdulillah tumeshinda pamoja kila pambano lililokuja mbele yetu.

“Muda wangu umemalizika na Asanteni sana.

“Tutaonana tena wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha juu ya jukwaa
“DaimaMbeleNyumaMwiko.

Mwenyekiti wa Wasemaji
Ally Kamwe.

Hata hivyo, Haji Manara baada ya kifungo chake kumalizika aliwaahidi mashabiki wa klabu hiyo kuitumikia tena kwa umahiri mkubwa katika nafasi ya msemaji wa timu hiyo.
Je, inawezekana Ali Kamwe kaogopa kufunikwa na Manara pale Yanga?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad