Polisi Nchini Kenya imepiga marufuku maandamano katika jiji la Nairobi ikisema wanalenga kuzuia makundi yenye nia hasi ya kutumia mwanya huo kutenda uhalifu.
Kauli hiyo inakuja kufuatia uhamasishaji wa mabango yaliyosambazwa mtandaoni yakihamasisha waandamanaji kukusanyika katika uwanja wa Uhuru Park uliopo jijini humo ili kuelekea Ikulu wakipinga utawala wa Rais Ruto.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa karibu Watu 50 waliuawa katika maandamano yanayoongozwa na vijana maarufu kama Gen Z wakipinga ongezeko la kodi lililopendekezwa na Serikali.
Muswada huo hata hivyo Rais William Ruto aliuondoa na kuvunja baraza lake la Mawaziri lakini hasira ziliamka tena maaba ya kupatikana kwa zaidi ya miili 20 iliyokuwa imefungwa kwenye viroba.