Kiama Chaja...Database ya Wauza Unga Tanzania Yakamilika....


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) imesema imekamilisha kanzidata (Data base) ya Wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na imeanza uchunguzi juu ya Watu hao.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 17,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema “Wengi wamebainika wapo ndani ya Nchi na wengine nje ya Nchi, baadhi yao wana biashara nyingine halali lakini wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kufanya utakatishaji”

“Mamlaka inatoa wito kwao kuachana mara moja na biashara hiyo na kujikita kwenye biashara halali kwani uchunguzi dhidi yao unaendelea”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad