Nimeona masimango mengi dhidi yangu kutoka kwa mbumbumbu! Sitochoka kutoa elimu ya bure. Muikatae sawa, muikubali sawa. Hakunaga elimu mbaya. Hakunaga ukweli ulioaibika, ni suala la muda tu kabla haujasimama na kujidhihirisha.
Ukweli hua una mwendo wa kinyonga, uongo una mabawa kama tai.
Kama hatujarekebisha mfumo na muundo wa timu yetu, hata mwekezaji aweke nini hakutokuwa na mafanikio ya kutisha! Kama ilivyo ada, kuna siku mtanikumbuka tena. Iko hivi, hakuna alichonacho tajiri mwenye elimu akakikosa.
Kilichofanyika ni kupaka rangi ufa, na siyo kurekebisha ukuta.
Kuna maneno ya dhihaka yakitaka mimi nisajili walau mchezaji mmoja tu! Kwa taarifa yenu mbumbumbu, mjue tu kuwa sishindwi! Huo msuli ninao. Mimi siyo maskini kiasi hicho. Kabla ya huu mchakato tulichangia sana mafanikio ya Simba SC, sema bila matangazo, sababu hatukuwa tukitafuta chochote.
Lakini, kwa wenye mantiki watahoji, kwamba nisajili kama nani? Ili iweje? Mfumo mpya umefeli? Najiuliza.
Najiuliza, mwekezaji kaweka bilioni 6! Lini? Mchanganuo wake uko wapi? Kaziweka kama kitu gani? Najiuliza.
Najiuliza mapato ya mwaka jana ni yepi? Anatangaza bidhaa zake kwa minajili ipi? Yeye ni Mwenyekiti wa Bodi, kwa minajili ipi? Hisa kalipia ama la? Jibu: Hajalipia. Anatoa wapi mamlaka na madaraka ya kuteua Bodi ilhali hajalipia hisa zake? Na kwa nini mbumbumbu mnafurahia? Ama kweli ni mbumbumbu? Najiuliza tu!
Najiuliza, miaka 7 imepita hatujakamilisha transformation! Why? Miaka 7! Tunakwamishwa na serikali ama na nani? Miaka 7! Najiuliza matangazo yake ya miaka 7 yanaingiza kiasi gani Simba? Zinatumikaje? Najiuliza.
Mniache nivune mpunga wangu niuze nipate hela mie. Mnanivuruga tu! #HK #Fighter #NjeYaBox #NguvuMoja"