KIKOSI cha Yanga Vs FC Augsburg Leo Tarehe 20 July 2024

KIKOSI cha Yanga Vs FC Augsburg Leo Tarehe 19 July 2024
KIKOSI cha Yanga Vs FC Augsburg Leo

KIKOSI cha Yanga Vs FC Augsburg Leo Tarehe 20 July 2024

Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka Uwanja wa Mbombela, uliopo Mpumangala Afrika Kusini kuvaana na FC Augsburg inayoshiriki Bundesliga ya Ujerumani, huku ikiwa imefikia na kujichimbia katika hoteli moja ya kishua itakayotumika kwa kambi ya siku 16 nchini huo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024-25.

Mchezo dhidi ya FC Augsburg ndio ambao utawafanya mashabiki wengi wa timu hiyo kuufuatilia kwanza ni kutokana na kutarajiwa kuonyeshwa mubashara na Azam TV, lakini ni mchezo unaotumika kutestia mitambo mipya iliyotua klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano ikiwamo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho (FA) na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilitua Afrika Kusini sambamba na Wajerumani hao wanaonolewa na kocha Jess Thorup ziote zikifikia Johanesburg, kisha zote mbili mbili zilianza safari ya kwenda Mpumalanga kwa maandalizi ya mwisho wa mechi hizo maalumu

"Itakuwa uzoefu wa thamani na wenye manufaa kwa timu nzima," alisema Mkurugenzi mkuu wa Augsburg Michael Stroll. "Tungependa pia kuchangia kuwakilisha Bundesliga nje ya nchi na kuinua hadhi yake ya kimataifa kwa kukaa kwetu Afrika Kusini."


FC Augsburg itajipima ubavu dhidi ya Yanga bila ya kuwa na nyota wao ghali zaidi mwenye thamani ya Sh. 26.2 bilioni, Rubén Vargas aliyefanya vizuri katika michuano ya mataifa ya Ulaya 'Euro 2024' iliyofanyika Ujerumani akiwa na timu ya taifa la Uswisi kwa sasa fundi huyo anamalizika likizo yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad