Kuhusu Kocha Mkuu Simba, Huyu Hapa Kula Shavu la Miaka Miwili




 UONGOZI wa Simba SC upo sokoni kutafuta mrithi wa Abdelhak Benchika ambaye aliondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, na majukumu yake kukaimiwana Juma Mgunda.

Makocha wengi wametuma CV zao Simba, lakini hadi sasa ni makocha wawili tu ndiyo wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuvaa viatu vya Mmoroco huyo.

Kuna Kocha aliyewahi kuifundisha Mamelod Sundowns Steve Komphela jina lake ndiyo likuwa la kwanza kabla ya upepo kubadilika siku ya jana.

Fadlu Davids amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Bodi ya Simba Sports Club, Salim Abdallah Muhene mazungumzo yao yamekuwa mazuri, anaweza akasaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha Simba.

Fadlu Davids ana umri wa miaka 43, Ni raia wa Afrika Kusini 🇿🇦 kwasasa ni kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco 🇲🇦.

Fadlu Davids ana Leseni ya Uefa Pro Licence, anapendelea mfumo wa 4-2-3-1.

Msimu wa mwaka 2018/19 na 2021/22 alikuwa Kocha msaidizi wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Msimu wa 2022/23 alikuwa Kocha msaidizi wa Locomotiv Moscow ya Russia 🇷🇺.

Msimu wa 2023/24 Kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco 🇲🇦 ambae ni hadi sasa.

Fadlu Davids amekuwa sehemu ya wanaounda benchi la ufundi la majerumani Joe Zinnbaeur ambae kwasasa ni kocha mkuu wa Raja Casablanca, mara zote anapoajiriwa kocha wake msaidizi ni muafrika Kusini Fadlu Davids.

Fadlu Davids ameshakuwa Kocha mkuu mara kadhaa akiwa na Kikosi cha Orlando Pirates pamoja na Martizburg United zote za Afrika Kusini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad