KUMEKUCHA: Mahakama Yaamuru Eng. Hersi Aondoke Yanga


KUMEKUCHA: Mahakama Yaamuru Eng. Hersi Aondoke Yanga


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.


Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.


Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.


Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne (hadi 2026) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad