Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu maandamano makubwa yaliyoshuhudiwa tarehe 18 hadi 27 kuitikisa nchi hiyo kiasi cha kusababisha vifo vya zaidi ya watu 39 kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu Kenya.
Awali vijana hao waliandamana kupinga kupitishwa kwa muswada wa fedha wa mwaka 2024 ambao tayari Rais Ruto amekwepa kuusaini na kuurudisha bungeni, huku akisisitiza kutaka mazungumzo na vijana hao.
Tayari maafisa wa polisi wanailinda barabara ya kuelekea Ikulu ya Nairobi huku Mahakama nchini humo pia ikiruhusu Jeshi la nchi hiyo KDF kuingia mtaani.
“Rais alituambia angeshusha bei ya unga, wakati akiingia ilikuwa Sh250 sasa ni Sh100 lakini ukweli ni kwamba unga sio Sh 100. Unga ni kitu Sh114. Nikiongea hivi naongea kama mtu ametoka kwa dukani jana,” amenukuliwa Henry Mchwenge muandamano kutoka Mombasa.
“Taswira ambayo tunajaribu kumpa rais ni kwamba tunataka kumsisitiza bado tuko na bado tunataka masuala yatatuliwe,” Henry Muchwenge – Mwekahazina wa Muungano wa bodaboda.