Mamelodi Sundowns Kiboko Sana, Waandaa BILIONI 4 Ofa ya Pili Kwa Fei Toto...

Mamelodi Sundowns Kiboko Sana, Waandaa BILIONI 4 Ofa ya Pili Kwa Fei Toto...
Fei Toto


Mamelodi Sundowns Kiboko Sana, Waandaa BILIONI 4 Ofa ya Pili Kwa Fei Toto...


Klabu ya Mamelodi Sundowns imepanga kutuma ofa ya pili kwa klabu ya Azam kwa ajili ya huduma ya Feisal Salum. Sundowns wanataka kuziba pengo la Bongani Zungu na Gaston Sirino ambao wametimka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Soccer Laduma (SNL), ofa ya kwanza ya Rand milioni 25 (TZS bilipni 3.7) ilikataliwa na mabosi wa Azam, na sasa wameandaa Rand milioni 32 (TZS bilioni 4.7) ili kupata huduma za kiungo huyo.

Inaripotiwa kuwa mazungumzo kati ya Azam na Mamelodi hayakusimama tangu ofa ya kwanza, lakini Azam wanahitaji angalau Rand milioni 36 (TZS bilioni 5.2) ili kumuachia Fei Toto.

Msimu uliopita wa 2023/24, Fei Toto alimaliza ligi akiwa na magoli 19 nyuma ya Aziz Ki aliyepachika nyavuni mabao 21. Hivi sasa yupo Morocco wakijiandaa na msimu mpya wa mashindano na tayari amefunga magoli 2 kwenye mechi moja ya kirafiki dhidi ya Zimamoto ya Zanzibar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad