Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt. Said A. Mohamed leo tarehe 13/07/2024 ametangaza Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu ngazi ya Cheti na Diploma 2024 ambapo ufaulu wa mwaka huu 2024 umepanda hadi asilimia 99.1
Aidha Dkt. Mohamed amesema Baraza hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 326 kutokana na sababu mbalimbali.
CLICK HERE TO GET THE SIXTH FORM RESULTS >>>
Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi, Julai 13, 2024 na Katibu Mtendaji wa Necta katika ofisi za baraza hilo Zanzibar, Dk Said Mohamed amesema watahiniwa walibainika kuingia na simu kwenye vyumba vya mtihani, kukutwa na notisi na wengine kusaidiana kufanya mitihani.
Kati ya waliofutiwa matokeo hao 24, amesema watahiniwa 22 ni wa kidato cha sita, 17 wa shule na watano wa kujitegemea, mmoja wa mtihani wa ualimu daraja A na mmoja wa stashahda ya ualimu.
Kwa mujibu wa Dk Mohamed, tathmini ya udanganyifu inaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na imani yao itafika wakati itakwisha.
Katibu Mtendaji huyo wa Necta, amesema ufaulu wa jumla kwa masomo yote ni asilimia 96.84 huku somo lililoonekana kuendelea kuwa mwiba kwa watahiniwa ni Basic Alliance Mathematics (BAM) ambalo ufaulu wake ni asilimia 78.
Katika matokeo hayo, Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 326, kati ya hao 304 wa mtihani wa kidato cha sita, 12 wa ualimu na tisa mtihani wa stashahada ya ualimu wa sekondari wamezuiliwa kutokana na matatizo ya kiafya.
Hata hivyo, Dk Mohamed amesema vitendo vya udanganyifu katika mitihani hiyo vimeendelea kudhibitiwa na kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
“Matukio ya udanganyifu wa kimkakati kwa sasa hayapo yameendelea kudhibitiwa na ndio maana unaona leo hata hatujatangaza shule yoyote ambayo imejihusisha na udanganyifu badala yake ni kutokana na wanafunzi wenyewe,” amesema Dk Mohamed.
Matokeo yalivyokuwa
Dk Mohamed amesema watahiniwa 113, 536 wa shule na kujitegemea walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei mwaka huu kati ya hao wasichana ni 50, 614 sawa na silimia 44.58 na wavulana 62,922 sawa na asilimia 55.42.
Kati ya watahiniwa hao watahiniwa wa shule walikuwa 104,454 na watahiniwa kujitegemea walikuwa 9,082.
Amesema kati ya watahiniwa 104, 454 wa shule waliosajiliwa watahiniwa 103,812 sawa na asilimia 99.39 walifanya mtihani, wasichana walikuwa 46,793 sawa na silimia 99.43 na wavulana ni 57, 019 sawa ana silimia 99.35. Watahiniwa 642 sawa na silimia 0.61 hawakufanya mtihani huo.