Meneja wa KIBU Denis Aeleza Alipo Mchezaji Wake

 

Meneja wa KIBU Denis Aeleza Alipo Mchezaji Wake

Meneja wa Wachezaji wa Ligi Kuu ya Tanzania Carlos MatserMind, ambaye pia ni meneja wa Kibu Denis Prosper.

IKIWA Sintofahamu juu ya mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis kutokuwepo kambini nchini Misri, Meneja na Msimamizi wa nyota huyo, Carlos Mastermind amesema nyota na hadai kitu chochote klabu hiyo na yupo Ulaya.

Kibu aliyeongeza mkataba wa miaka miwili, bado hajajiunga na timu hiyo iliyopo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hali ambaye imeleta maswali mengi lakini wenye Simba yao wameamua kuliweka wazi.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, amesema anachofahamu nyota huyo alikuwa Tanzania kukabiliana na changamoto za hati yake ya kusafiria na baadae ameenda Ulaya.

Amesema Kibu alienda Ulaya kwa ajili ya mapumziko na familia yake, akarejea nchini na kufatilia hati ya kusafiria ilikuwa na changamoto baadae akapata matatizo ya kifamilia na kwenda Kigoma.

“Ni kwelu kibu hajajiunga na timu Misri kwa sasa yupo Ulaya, ninachojua kuwa hawadai Simba wamemalizana na suala la kwanini hajajiunga na wenzake nchini Misri, Simba wanauwezo wa kulijibu hilo,” amesema Carlos.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally umeweka wazi kwamba hati ya kusafiria ndiyo kikwazo cha mshambuliaji wao Kibu Denis kutokujiunga kambini na timu hiyo iliyo nchini Misri.

Amesema nyota huyo hana shida na uongozi bali amekutana na changamoto zake binafsi ikiwamo hati yake ya kusafiria kujaa na anatarajiwa kuungana na wenzake kambini mapema wiki hii kwa ajili ya kuendelea na maandalizi wakati huu wakijiandaa na Tamasha lao la Simba Day.

Amesema Mchezaji huyo haidai Simba kitu chochote kama baadhi ya wadau wa Soka wanavyodhani na badala yake tatizo kubwa ni hati yake ya kusafiria jambo ambalo wanaendelea kulishughulikia kwa ukaribu zaidi.

“Kibu haidai Simba chochote kama wengine wanavyodhani, ila hati yake ya kusafiria imejaa anafanya mchakato, aliomba ruhusa ya kuchelewa kujiunga kambini kutokana na changamoto hiyo na tukamuelewa ila tunatarajia kumuona muda wowote,” amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad