Diamond Platnumz sasa ni msanii wa muziki wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara mwenye subscribers wengi zaidi kwenye YouTube, zaidi ya milioni 9.
Mwanzo wa Safari: Alijiunga na YouTube Juni 12, 2011. Video ya kwanza kabisa aliyochapisha ilikuwa ya mapokezi yake Songea, iliyotazamwa mara elfu 27.
Video ya Kwanza ya Muziki: “Utamu” ya Dully Sykes, Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz - imetazamwa mara milioni 1.4. Video hii inakumbusha urafiki na ushirikiano wa zamani kati ya Diamond na Ommy Dimpoz.
Video ya “Kesho” iliyotolewa Desemba 29, 2012, imekusanya watazamaji zaidi ya milioni 4.3. “Muziki Gani” aliyoshirikishwa na Nay wa Mitego imetazamwa mara milioni 3.2 tangu Mei 27, 2013. Video za “Muziki Gani” na “Utamu” zinaonyesha safari ya Diamond Platnumz kuunga mkono wasanii wenzake ilianza kabla ya ukubwa alionao sasa.
Video za wasanii aliowakuta kwenye gemu ziliachiwa kupitia chaneli yake kutokana na ushawishi alionao kipindi hicho kama msanii mpya aliyekuwa akiakisi maisha anayoyaishi sasa.
Mafanikio na Kolabo Kubwa:
“Yope Remix” na Inno’s B - 231M views, iliyotolewa Septemba 7, 2019.
“Waah” na Koffi Olomide - 159M views, iliyotolewa Novemba 30, 2020.
“Inama” na Fally Ipupa - 137M views, iliyotolewa Juni 9, 2019.
Ushirikiano wake na wasanii wa Kongo umeonyesha uwezo wake wa kuvuka mipaka na kutengeneza nyimbo maarufu duniani.
Uendelevu na Ubunifu: Diamond ameendelea kuvutia watazamaji kwa maudhui yake ya kipekee na ubora wa video zake. Anawasiliana moja kwa moja na mashabiki wake, akiwapa kile wanachotakiwa kuona kwa ubunifu wa hali ya juu.
Views Bilioni 2.6: Kwa zaidi ya miaka 13, Diamond ameweza kufikisha views zaidi ya bilioni 2.6 kwenye channel yake, kitu ambacho ni nadra kufikiwa na wasanii wengi wa Afrika.
Maudhui Anayotoa: Ameweza kutoa maudhui yanayovutia kama vile video za muziki, matukio, na maisha yake binafsi, yote haya yakionyesha juhudi zake na ubunifu wake katika muziki.
Kazi Inayo-trend Sasa: “Komasava (Comment Ça va)” na Chley na Khalil Harrison - tayari imeshapata watazamaji zaidi ya milioni 3. Wimbo huu unazidi kuonyesha jinsi Diamond anavyoendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika muziki wa Afrika
SNS