"Gamondi ni Kocha mkubwa na anao uzoefu wa kufanya kazi na wachezaji wakubwa,siku zote sisi makocha kwenye timu huwa kuna mchezaji huwa anakuwa kipenzi chako kwakuwa anafanya kitu cha ziada,anatumia akili zaidi hata ya maarifa ya mwalimu,na anakuwa na nidhamu,utajikuta unampenda.
Sasa kwa Yanga wanao wachezaji wenye vipaji,na wanacheza kwenye maeneo yanayofanana, Gamondi anapaswa asioneshe mapenzi kwa mchezaji anayempe da,atengeneze mpango wa kuwatumia vizuri Aziz Ki,Pacome Zouzoua na Clatous Chama,iwapo kuna mmoja atakosa nafasi anaweza kumshushia mmoja kiwango kwa kukosa fitness halafu akajenga chuki kwa Kocha,na hawa Wachezaji wazuri mara nyingi ni vipenzi kwa Viongozi, anaweza kumchongea halafu Gamondi akawa wa kwanza kuondoka"Charles Boniface Mkwasa Kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga!
Vipi wanangu,unampa miezi mingapi Miguel Gamondi ?