Mwamba Aliyechoma Picha ya Rais Aachiwa Huru


Mwamba Aliyechoma Picha ya Rais Aachiwa Huru


Kijana Shadrack Chaula (24) Mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Tsh. milioni 5 kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni na kuchoma picha ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameachiwa huru baada ya kufanikiwa kulipiwa faini na Wananchi ambao walichangia pesa hizo.


Kijana huyo alihukumiwa Alhamisi July 4, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro.


Akiongea baada ya kuachiwa, Shadrack amesema “Asanteni Ndugu zangu Watanzania, asante Ndugu zangu Mawakili kadhaa wa kadhaa kwa kunitetea na nawashukuru umoja wa Watanzania wote mliosimama vikali kuhakikisha mnanitetea asanteni sana na Mungu awabariki”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad