Sakata la Kibu Dennis limeingia sura mpya baada ya kubainika kuwa yupo Nchini Norway kwa ajili ya majaribio baada ya kuitoroka Simba Sc kama ilivyoripitiwa awali.
Hii ni baada ya nyota huyo kupokea barua ya mwaliko kutoka klabu ya Kristiansund BK ya Nchini humo kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya Mwezi mmoja kuanzia tarehe 08 Julai 2024 mpaka 08 Agosti 2024.
Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa ina miaka 20 tu na ina uwanja wake wenye uwezo wa kubeba watazamaji 4,444 walioketi na imepanda daraja msimu uliopita sasa inacheza ligi daraja la kwanza nchini humo.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Isamil Aden Rage amewaomba Viongozi wa Simba SC kutomng'ang'ania Kibu Denis.
"Kibu Denis ameonyesha kutokua mwaminifu na huenda akawa sehemu ya wahujumu Simba SC msimu unaofuata. Viongozi wa Simba hawapaswi kumng'ang'ania.
"Nawasihi viongozi wa Simba wasimkomoe mchezaji bali atakaporejea wazungumze naye ili kila upande unufaike kulingana na makubaliano lakini wamruhusu aende zake.
"Mimi niliwahi kukutana na kesi kama hiyo nilipokua katika harakati za kumsajili Mbuyu Twite ambaye licha ya kumpatia dola elfu (40) lakini akasaini pia na Yanga SC ambapo ili kuepusha mgogoro tulimueleza arudishe pesa tulizompa na kuongezea dola elfu tano," amesema Rage.