Pigo Kubwa Kwa Simba, Kiungo Mkabaji Yusuph Kagoma Kuikosa Mechi ya Yanga

 

Pigo Kubwa Kwa Simba, Kiungo Mkabaji Yusuph Kagoma Kuikosa Mechi ya Yanga

Kiungo mkabaji wa Simba, Yusuph Kagoma (28) atakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili hadi tatu baada ya kupata majeraha akiwa kambini Ismailia, Misri.

Kagoma ni kati ya wachezaji ambao wamesajiliwa na Simba katika dirisha kubwa la usajili akitokea Singida Fountain Gate katika msiu uliopita.

Hadi hivi sasa bado taarifa rasmi haijatolewa majeraha ambayo ameyapata akiwa kambini huko wakijiandaa na msimu ujao, hivyo kiungo huyo atakosekana katika Kariakoo Dabi itakayopigwa Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ngao ya Jamii, mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana, Simba ilipoteza mchezo kwa mabao 2-1, huku mzunguko wa kwanza wa msimu  wa 2023/24 Simba ilichapwa 1-5.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad