Baada ya kutangaza kujiengua kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Marekani, Rais wa Nchi hiyo, Jose Biden amempigia upatu Makamu wa Rais Kamala Harris kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 2024.
“Leo nataka kutoa uungwaji mkono wangu kamili na uidhinishaji kwa Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu “Democrats – ni wakati wa kukusanyika na kumpiga Trump.”,” amesema Biden katika chapisho lingine kwenye mtandao X.
Hata hivyo mwanamama huyo anakabiliwa na mashaka makubwa juu ya uwezo wake wa kushinda Urais huo au kufanya vizuri ikiwa atarithi nafasi hiyo.
Kura ya maoni ya asubuhi ya leo imefichua kwamba ni theluthi moja tu ya wapiga kura wanafikiri kuna uwezekano Harris angeshinda uchaguzi ikiwa atakuwa mgombea mteule wa Chama cha Democratic Kidemokrasia.
Kura ya maoni imeonyesha kuwa kama ilivyokuwa kwa Biden, uwezekano wa Harris kuibuka kidedea ni mdogo huku akipata asilimia 42 tu za kukubalika na 52 za kukataliwa.