Rais Samia Akerwa na Waziri na Katibu Kugombana



Waziri wa Madini, Anthony Mavunde
RAIS Samia Suluhu Hassan ameeleza kukerwa na ugomvi kati ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Kheri Abdul Mahimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema haelewi ni kwanini waziri na katibu mkuu wake wanagombana na wanagombea kitu gani wakati kila mtu ana majukumu yake.


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Kheri Abdul Mahimbali.
Rais Samia ametoa hayo ya moyoni leo Ijumaa wakati akimfunda Mhandisi Yahya lsmail Samamba baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini. Pia amewaapisha viongozi wengine wateule katika Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar.

Tarehe 2 Julai mwaka huu, Rais Samia alimteua Mhandisi Samamba aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini kuchukua nafasi ya Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Amesema hakuna mwenye sekta yake peke yake hivyo viongozi hao walioaposhwa wanapaswa kujua kuwa cheo ni dhamana na wote tunajenga Tanzania hivyo hakuna haja ya kuvuragana.


Mhandisi Yahya Samamba
“Huwa sielewi kwanini waziri na katibu mkuu wanagombana kitu gani, kwa sababu kila mtu na majukumu yake.

“Samamba nimekutoa tume ya madini umefanya vizuri. Unaijua vizuri sekta ya madini pili STAMICO tumefanya uwekezaji mkubwa sana nenda kaisimamie,” amesema.

Amesema kinachomuumiza kichwa ni leseni nyingi za madini zilizotolewa kwa watu ambao wamezihodhi bila kufanya uwekezaji wowote.

Pia alimtaka kwenda kuhakikisha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) inakwenda kuongezewa nguvu na kupima eneo lote la madini.

Pamoja na mambo mengine amemtaka Katibu mkuu huyo kwenda kuziba mianya ya utoroshaji madini kwani hakuna sababu ya kuwepo kwa uhaba wa dola ilihali madini ya kutosha yapo Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad