Rais Samia Aridhia Ombi La Kinana Kujiuzulu Nafasi Ya Makamu Mwenyekiti Wa CCM



Rais Samia Aridhia Ombi La Kinana Kujiuzulu Nafasi Ya Makamu Mwenyekiti Wa CCM

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.


Kulingana na taarifa ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM taifa Amos Gabriel Makalla iliyotolewa Julai 29, 2024 Rais Samia ameridhia ombi la Kinana kujiuzulu kutokana na ahadi aliyomuahidi Kinana ya kuridhia kujiuzulu kwake.


“Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako” Amenukuliwa Rais Samia katika taarifa ya Makalla.


Aidha Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila vitakapohitajika huku CCM ikimshukuru Abdulrahman Kinana kwa mchango wake uliotajwa kuwa mkubwa kwa chama hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad