Rais wa Marekani Joe Biden Ajitoa Kinyang'anyiro Uchaguzi Marekani




Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa atasitisha kuwania tena uchaguzi wa urais akisema ni kwa manufaa ya 'chama changu na nchi'. Hatua yake inakuja miezi minne kabla ya Wamarekani kupiga kura, na kusimamisha azma yake katika kinyang'anyiro cha kuwania muhula mwingine katika Ikulu ya White House.

Inafuatia wiki za shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa Democratic baada ya matokeo yake mabaya katika mdahalo ulioyumba dhidi ya Donald Trump wa chama cha Republican mwishoni mwa Juni.


Katika barua iliyotumwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, alisema imekuwa heshima kubwa maishani mwake kuhudumu kama rais.

"Na ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa na kuzingatia tu kutimiza wajibu wa Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wangu".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad