Rapa Wakazi akosoa wanao diss kolabo ya Diampnd na Jason Derulo



Rapa Wakazi akosoa wanao diss kolabo ya Diampnd na Jason Derulo, wakidai kwamba kwa sasa msanii huyo wa Marekani hana maajabu.

Wakazi amesema, "Kulikuwa hamna haja ya ku-diss the feature. Watu hawafanyi collabo just because fulani is the trending artist. Jason ana mashabiki wake wanaomsikiliza na pengine baadhi hawakuwa mashabiki wa Diamond; na kinyume chake ni kweli."

Aliendelea, "Turudi kwenye kufurahia muziki mzuri. Kwenye collabo, kinachohesabika ni chemistry na delivery, sio jina wala umaarufu. Je, wamefanya vizuri? Wametisha? Basi."

Wakazi pia ameweka wazi ndoto zake za kufanya kazi na wasanii kama Coumba Gawlo na Joss Stone, akisema hata kama hawajulikani sana, ataenda kwao kabla ya mastaa wenu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad