Shilole "Wadogo zangu Nani Kawadanganya Kuwa na Makalio Makubwa Ndio Kufanikiwa Mjini?"


Shilole "Wadogo zangu Nani Kawadanganya Kuwa na Makalio Makubwa Ndio Kufanikiwa Mjini?"


"Wadogo zangu nani kawadanganya kwamba kuwa na makalio makubwa ndio kufanikiwa?" - Shilole "Kwa Wadogo zangu, na Watoto wangu, Nani aliwadanganya kuwa na makalio makubwa ndio kufanikiwa? Nani aliwadanganya kufanya mambo ambayo hayampendezi maulana ndio kufanikiwa?

Wakati natoa #NakomaNaJiji mengi yalikuwa yakizungumzwa, Wengi walisema nirudi kwetu Igunga kwasababu huu mji nimeushindwa, Nilichoimba kwa wakati huo ulikuwa ni ukweli mtupu ilifika kipindi nilikuwa ninazungumza na Mungu wangu tu, Yatima mimi ambaye kutafuta sijachoka, Mungu alinijalia sikuweza kuanguka.

Nani aliamini kwa kipindi kile nitaweza kufungua mgahawa wa chakula mkubwa na kufanya vizuri kila kona. Jiulize ni watu wangapi maarufu walianzisha biashara na wakashindwa kusimamia? Tazama shishifood na ujifunze.

Somo langu kubwa kwa wadogo zangu na watoto wangu, Hii dunia imejaa kila aina ya watu jitahidi uwe moja kati ya watu wema, Jitahidi uwe hadithi nzuri siku ukiondoka : Mimi ni hamasa kwa kundi kubwa la Wanawake wenye ndoto wale wanaopitia magumu sana, Wale wanaotoka hali ya chini sana." - Shilole

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad