Treni ya SGR Yasimama Muda wa Masaa Mawili Njiani, TRC Watoa Ufafanuzi na Kuomba Radhi

Treni ya SGR Yasimama Muda wa Masaa Mawili Njiani, TRC Watoa Ufafanuzi na Kuomba Radhi


Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili usiku wa jana July 30, 2024.


Taarifa iliyotolewa leo July 31,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano - TRC, Jamila Mbarouck imesema “Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system)”


“Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku”


“Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku, Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad